25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MDEE APEWA SAA NYINGINE NA POLISI

Na PATRICIA KIMELEMETA

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), bado anaendelea kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam, licha ya saa 48 zilizotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kumalizika juzi usiku.

Sababu za Polisi kuendelea kumshikilia mbunge huyo  ambaye leo anatimiza siku ya nne ndani ya selo za Jeshi hilo bado hazijafahamika.

Mdee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), alikamatwa Julai 4, mwaka huu, baada  ya  Hapi, kutoa amri ya kushikiliwa kwa saa 48 kutokana na matamshi aliyodai kuwa ni ya kumkashifu Rais Dk. John Magufuli.

Matamshi hayo ni yale  anayodaiwa kuyatoa katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, yaliyopo Kinondoni, Dar es Salaam.

MTANZANIA Jumamosi ambalo lilitaka kufahamu sababu za Jeshi hilo kuendelea kumshikilia Mdee liliwasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Susan Kaganda ambaye alithibitisha kuendelea kumshikilia mwanasiasa huyo kituoni hapo lakini alikataa kueleza sababu.

“Bado tunamshikilia hadi leo (jana) kutokana na agizo lililotolewa na DC, lakini taarifa zaidi atakayezitoa ni Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,” alisema Kaganda.

Alipoulizwa ni kwanini wanaendelea kumshikilia licha ya saa 48 alizopewa kumalizika tangu juzi saa 12 jioni, Kaganda alisema kwa kifupi na kisha kukata simu; “Mimi naendelea kumshikilia hilo suala aulizwe Kamishna Kanda maalumu”.

Zipo taarifa zinazodai kuwa Mdee aligoma kula kama njia ya kushinikiza kufikishwa mahakamani ili vyombo vya sheria .

Mdee alikamatwa kwa amri ya Mkuu huyo wa Wilaya kwa kile alichodaiwa kumkashifu Rais Magufuli kutokana na kuhoji baadhi ya kauli zake zikiwemo zile alizotumia wakati akitangaza kupiga marufuku wanafunzi wa kike wanaopata mimba kurejea shuleni.

Si hilo tu Mdee pia alihoji kauli nyingine zinazotolewa na Rais Dk. Magufuli ambazo alidai kuwa zinakiuka misingi ya sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles