23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Mdee amuuguza Bulaya ashindwa kufika mahakamani

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee, ameshindwa kuhudhuria katika kesi inayomkabili ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Dk. John Magufuli, kwa sababu anamuuguza Mbunge mwenzake Esther Bulaya.

Kesi hiyo ilishindwa kuendelea na ushahidi jana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  kuelezwa sababu hizo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita alidai  kesi ilikuja  kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mshtakiwa hakuwepo mahakamani.

Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu alidai kuwa amepewa taarifa na wadhamini wa Mdee, Phares Rutomo kuwa,  mshtakiwa anamuuguza Mbunge  wa Bunda, Esther Bulaya.

Rutomo alizungumza na Mdee  na kumueleza kuwa anamuuguza Bulaya ambaye, amelazwa katika hospitali ya Bunge iliyopo jijini Dodoma

Hata hivyo, Rutomo aliiambia mahakama hiyo kuwa, kwa sasa Mdee anamuuguza,  Bulaya nyumbani kwake.

“Taarifa hii inaleta ukakasi, kwa maelezo haya,  nina wasiwasi kama kesi hii itamalizika kwa wakati, kwa sababu hali hii inakwaza, ” alisema Hakimu Simba.

Alisema mahakama ikiruhusu mambo yanedelee kama haya, kesi hiyo haitakamilika kwa wakati.

Simba alisema mahakama haina tatizo kama mtu amepata udhuru, lakini wakati mwingine huwa wanaionea mahakama.

Hakimu Simba, aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 28, 2019, kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Katika kesi ya msingi, inadaiwa kuwa Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki”  na kwamba kitendo hicho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles