25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Mdee ahoji ahadi Wizara ya Ardhi kutengeneza miundombinu Kawe

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema)  amehoji  ni kwanini wananchi wa Kawe hawatengenezewi miundombinu licha ya kulipia.

Akiuliza swali jana bungeni, Mdee alidai kwamba Wizara ya Ardhi kupitia mradi wa viwanja 20,000 iliuza viwanja kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Mdee alidai katika Jimbo la Kawe mradi huo ulitekelezwa kata za Mbweni na Bunju, wananchi walilipia viwanja kwa maelekezo kwamba gharama za viwanja zingetumika kuboresha miundombinu mbalimbali katika eneo husika.

“Lakini ahadi hiyo haikutekelezwa kwa ufasaha hali inayopelekea kero kubwa ya mafuriko na kutuama kwa maji, hususan kipindi cha mvua, kero kubwa ikiwa ni Mtaa wa Mbweni Feta na Mbweni Malindi. Je, ni lini Serikali itatatua kero hii?” aliuliza.

Ikijibu swali hilo, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilieleza ni kweli  kati ya mwaka 2003 na 2008, Serikali ilitekeleza mradi wa upimaji viwanja 20,000 maeneo mbalimbali katika wilaya za Dar es Salaam.

Maeneo hayo, ni pamoja na Bunju, Mivumoni, Mbweni JKT na Mbweni Malindi Manispaa ya Kinondoni.

 “Jukumu la Wizara lilikuwa ni kufungua barabara kwa mujibu wa michoro ya mipango miji na upimaji. Baada ya barabara hizo kufunguliwa zilikabidhiwa katika Halmashauri husika ambako viwanja hivyo vipo ili waziendeleze zaidi na kuzihudumia.

“Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha  mitaa ambayo viwanja hivyo vimepimwa inapitika wakati wote ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

 “Kwa sasa Serikali imeanzisha Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini, mamlaka hii imeendelea kutekeleza zoezi la urekebishaji wa miundombinu kwa maeneo yanayohitajika mfano zoezi linaloendelea katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni katika viwanja vya mradi eneo la Mwongozo,” ilieleza wizara hiyo.

Iieleza  kuwa wajibu wa Serikali ni kuwaonyesha watekelezaji ramani za viwanja ili kuweka miundombinu kuendana na mpango.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles