26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Mdee achangisha milioni 2.3/- kujenga daraja

mdeeMANENO SELANYIKA NA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), amefanya harambee kwa wananchi wa Kata ya
Bunju ‘A’ jijini Dar es Salaam ili kupata fedha za kujenga daraja.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika mkutano na wananchi, Mdee alisema fedha hizo zitatumika kujenga daraja katika kata hiyo ili kutatua kero ya usafiri kwa wananchi hao hasa kipindi cha mvua.
Mbali na harambee hiyo, Mdee aliwaahidi kuwapatia wakazi hao Sh milioni 5 kutoka mfuko wa jimbo ili kukamilisha ujenzi huo.
“Hii barabara ni kwa ajili ya matumizi ya jamii nzima hivyo ni jukumu
letu sote kuchangia, naamini mtaniunga mkono kabla ya sikukuu ya Krismasi kalavati ziwe zimeshawekwa, lakini ili tufanikishe jambo hilo ninawaomba wananchi mtoe fedha hizo mlizoahidi,” alisema Mdee.

Wakizungumzia kero zao kwa mbunge huyo, baadhi ya wananchi wa eneo hilo walisema mbali na kero ya miundombinu ya barabara wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama pamoja na shule.

Maua Shaweji, mkazi wa Gurumawe alisema wapo watu wenye uwezo wa kuunganishiwa maji hadi kwenye makazi yao lakini wanawanyanyasa kwa kuwauzia ndoo moja au mbili tu za maji.

“Mimi ninaishi hapa tangu mwaka 1974, tumenyanyasika sana na maji
tulidhani kwa kuwa watu wenye uwezo wamefika mtaani kwetu tungepata
ahueni ya tatizo la maji badala yake ni tatizo zaidi kwani ukienda kuomba maji unapewa ndoo mbili tu ambazo huwezi kuzitumia ukiwa na
familia,” alisema Maua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles