24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MCT wajadili usalama wa waandishi wa habari 

AMINA OMARI-TANG



BARAZA la Habari Tanzania(MCT) kwa kushirikiana na wahariri  na wadau wa habari nchini linaandaa  mpango kazi wa  uhuru wa habari   na mikakati ya kumaliza changamoto za usalama kwa waandishi wa habari nchini.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la hilo, Kajubi Mukajanga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa ushauriano kati yaMCT, wahariri na wadau wa habari nchini,   Tanga jana.

Alisema   mpango huo ndiyo utakaoweza kuwa suluhisho au ufumbuzi wa changamoto za usalama wa waandishi na kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari  nchini.

Kajubi alisema   anamini   mikakati hiyo ya pamoja itaweza kuweka dira ndani ya vyumba vya habari katika kuhakikisha wanasimama katika misingi yao ya haki katika kutimiza wajibu wao wa kuhabarisha umma kwa uhuru bila ya vikwazo vyovyote.

“Taifa linalozungumza  ni lazima litazame wale wanaozungumza  kama wana uwezo wa kuzungumza  kwa kuhakikisha uhuru wa uhariri na usalama wa waandishi unakuwa bora zaidi,” alisema Mukajanga.

Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari  (UTPC),  Jane Mihanji alisema waandishi  ambao wapo huru   wanaweza kutekeleza majukumu yao bila ya hofu yoyote.

“Tunatamani siku moja waandishi   nchini tuweze kufanya kazi kwa uhuru bila kuwa na woga wa kutishiwa maisha yetu wala kubanwa na mamlaka za juu katika kutekeleza majukumu yetu,” alisema.

Aaliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari, Absalom Kibanda alisema   kukithiri kwa unyanyasaji na vipigo kwa waandishi wa habari bila kuchukuliwa   hatua stahiki   ni pigo kwa tasnia nzima.

“Hatua ya kufungia vyombo vya habari siyo tu vinawaathiri waandishi ambao ni waajiriwa wa vyombo hivyo bali hata wananchi ambao walitegemea kupata habari kupitia vyombo hivyo,” alisema Kibanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles