26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Mchungaji, wenzake 550 waomba kibali kuishitaki Rita

NA KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

MCHUNGAJI wa Kanisa la EAGT, John Nchambi na wenzake 550 wamewasilisha maombi Mahakama Kuu akiomba kibali cha kuruhusiwa kumshtaki Msajili wa Wakala ya Msajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) na wenzake. 

Mchungaji huyo na wenzake wamefungua maombi hayo na 48 ya mwaka huu jana dhidi ya Msajili Rita,  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mchungaji Joshua Wawa, Christomoo Ngowi, Kenneth Kasunga na Peter Madaha. 

Waombaji hao wanaomba mahakama ifute uteuzi wa bodi ya wadhamini ya Kanisa la EAGT kwasababu kulikuwepo na zuio la msajili wa vyama vya kiraia la Machi 5 mwaka 2018 la kuzuia mikutano yote ya kikatiba ya kanisa hilo ambapo hadi sasa zuio hilo halijatenguliwa. 

Pia wanadai Msajili wa Rita ndiyo mwenye mamlaka ya kufanya uchunguzi dhidi ya ubadhilifu na matumizi mabaya ya mali za kanisa hilo lakini hadi  sasa zoezi hilo  halijakamilishwa na bodi ya wadhamini ikateuliwa huku miongoni mwa walioteuliwa alikuwepo katika bodi ya awali. 

Wanadai msajili wa Rita ameshindwa kutekeleza majukumu yake kisheria. 

Kwamujibu wa wakili anayemkwakilisha Nchambi na wachungaji wenzake 550, Robert Rutaihwa alisema katika barua ya Agosti 4 mwaka huu iliyotolewa na Rita, aliwatambua Wachungaji Joshua, Ngowi, Kasunga na Madaha kwamba kwasasa ndio wanaounda bodi ya wadhamini ya EAGT. 

Pia kupitia barua hiyo, Rita imetambua mgogoro uliopo juu ya ubadhilifu na usimamizi mbaya wa mali za kanisa hilo na kueleza kwamba tayari ameshaunda kamati ya uchunguzi, imeshafanya kazi na ipo katika hatu za mwisho kukamilisha taarifa ya uchunguzi huo. 

Kufuatia barua hiyo, baadhi ya wachungaji wakiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo wameitisha  mkutano mkuu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya sita ya kanisa hilo kuchagua viongozi wa kanisa la EAGT wakati kuna barua ya Machi 5 ya mwaka 2018 kutoka kwa msajili wa vyama vya kiraia inayozuia mikutano ya kikatiba, vikao na utekelezaji na kwamba barua hiyo haijawahi kitenguliwa. 

Alidai, Juni 28 mwaka 2019, wakati kukiwepo na zuio hilo, wachungaji hao walikaa na kuteua bodi ya wadhamini na kisha kupitishwa na Rita kinyume na taratibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles