30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MCHUNGAJI RWAKATALE AMSHUKURU JPM

Na Veronica Romwald-Dar es Salaam


MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto  lililopo Mikocheni B,  Assembles of God, Dk. Getrude Rwakatale, amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumkumbuka na kumteua katika nafasi ya ubunge wa Viti Maalumu.

Dk, Rwakatale alitoa shukrani  hizo Dar es Salaam jana wakati alipozungumza katika kanisa hilo wakati wa ibada ya Sikukuu ya Pasaka.

“Leo (jana) tunasherehekea kumbukumbu ya kufufuka kwa mwokozi wetu Yesu  ambaye alitufia pale msalabani,… Pasaka ya mwaka huu ni yangu, Mungu ameniona.

“Nina furaha ya mwili na roho kwa sababu Yesu amefufuka na pia Mungu amenirudisha bungeni, Mungu amejibu maombi yetu, tulifunga siku tatu na ile ya mwisho akajibu,”  alisema Mchungaji Rwakatale.

Alisema ana kila sababu ya kumshukuru Rais Dk. Magufuli kwa sababu  wapo wanawake wengi ambao angeweza kuwachagua na kuwapa nafasi hiyo.

“Nakishukuru pia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kunikumbuka, wapo wanawake wangapi lakini leo mlima wa moto katikati ya maombi, Mungu ametenda,” alisema.

Dk. Rwakatale alitumia ibada hiyo kuwaomba msamaha watu aliowakosea huku akiwasihi waungane naye kumshukuru Mungu katika maombi.

“Katika Luka 24:1-9 tunasoma habari kuhusu ufufuko wa Yesu, tumezoea makaburini huwa kuna habari mbaya lakini kwa Yesu ilikuwa tofauti, ilikuja habari njema.

“Alitangaza msamaha hata alipokuwa msalabani basi naomba mnisamehe nilipokosea maana na mimi ni mwanadamu,”  alisema.

Aprili 14, mwaka huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  kupitia kwa Mkurugenzi wa tume hiyo, Ramadhan Kailima ilitangaza jina la Mchungaji Rwakatale kuwa mbunge baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupeleka jina lake.

 Tume ilipitia  fomu zake na kuridhika kuwa mteule huyo ana sifa za kuwa mbunge akichukua nafasi ya Sophia Simba ambaye alivuliwa uanachama na chama chake.

Machi 11, mwaka huu, Sophia Simba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) alivuliwa uanachama kwa madai ya ukiukwaji wa maadili ya chama hicho na hivyo kumfanya kukosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles