26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

MCHUNGAJI MSIGWA AMMWAGIA SIFA JPM

Na MWANDISHI WETU-IRINGA


MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), amemsifu Rais Dk. John Magufuli akisema  ni kiongozi anayeongoza serikali bila kubagua vyama.

Kauli hiyo aliitoa juzi usiku mjini hapa wakati wa hafla ya chakula cha jioni  ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa wakiwamo madiwani wa vyama vyote.

Msigwa alimshukuru Rais Magufuli kwa akisema ni kiongozi wa mfano kwa sababu  amekuwa akiendesha serikali bila kubagua vyama  na kupeleka maendeleo katika maeneo yote ikiwamo Iringa

Alisema katika   miaka miwili na nusu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Rais Magufuli amedhihirisha kutanguliza masilahi ya Watanzania wote bila kubagua vyama vya siasa.

“Rais umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa wewe hujali mambo ya vyama  na hii imedhirika kuwa kweli hujali vyama, umesaidia sana, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi, kama alivyosema Mheshimiwa  Mahiga  kuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais.

“Umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu Sh bilioni 3.5, tuna stendi nzuri ipo Ipogolo ya karibu Sh bilioni tatu…tuna maji.

“Kwa hiyo kuna vitu vimefanyika kwa kweli Mheshiwa Rais hupendelei, hela zinakuja hata sisi ambao ni wa Chadema unaleta hela, kwa hiyo tunakupongeza sana,” alisema Mchungaji Msingwa.

Viongozi hao walimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada kubwa alizozielekeza katika kutekeleza miradi mikubwa ya  taifa ikiwamo ununuzi wa ndege kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ambayo itaimarisha utalii na kuitangaza nchi kimataifa, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge).

Mingine ni mradi wa umeme wa mto Rufiji (Stieglers’ Gorge), ujenzi wa viwanja vya ndege, bandari, barabara na madaraja, ambavyo vitaimarisha uchumi na kujenga heshima ya nchi.

“Rais nchi yetu ina vivutio vya utalii, ina rasilimali nyingi, haya unayofanya sasa yanakwenda kuitangaza nchi yetu, ndege zetu zinaporuka zikiwa zimechorwa mnyama Twiga na zimeandikwa ‘The Wings of Kilimanjaro’ zinaitangaza nchi yetu, treni itainua uchumi wetu, tunakupongeza sana na tunakushukuru sana,” alisema Salim Asas, Mjumbe wa NEC na Kaimu Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, mawaziri, viongozi wa dini, viongozi wa Wahehe, wabunge, madiwani, viongozi wa TUCTA, wafanyabiashara na viongozi wa Mkoa wa Iringa.

Rais Magufuli aliwashukuru viongozi hao na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Mkoa wa Iringa kusukuma maendeleo ya mkoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles