Mchungaji ataka Amberruty asitengwe

0
1418

Lulu Ringo, Dar es salaam      

Mchungaji wa Kanisa la Emmaus Bible, Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Daudi Mashimo aliyemdhamini mahakamani mcheza video za wasanii (video vixen), Rutfiya Abubakary(Amber Rutty), amesema mtuhumiwa huyo hana makosa makubwa ya kusababisha atengwe na jamii au kunyooshewa mikono na watu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Novemba 28, Mchungaji huyo amesema haoni sababu za kila mtu kumsakama Amber Rutty kwa maneno kwa kuwa wapo watu wenye maovu zaidi yake na wengine ni watumishi wa Mungu.

“Amber Rutty ni mtoto wa Mungu, na mimi nimefarijika sana nilipomuwekea dhamana, huyu dada hajafanya kosa la kumfanya atengwe na jamii wapo watu wengi waovu tena wengine ni watumishi wa Mungu ambao ninyi mnawaamini,” amesema Mashimo.

Amber Rutty na mpenzi wake Said Bakary walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 2, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here