24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MCHUNGAJI APATA ALMASI YA MAMILIONI YA DOLA

Freetown, Sierra Leone


MCHUNGAJI wa kikiristo amepata moja ya almasi kubwa zaidi ambayo haijawahi kupatikana duniani.

Mchungaji huyo anayejulikana kwa jina la Emmanuel Momoh amepata almasi hiyo katika Wilaya ya Kano nchini Sierra Leone.

Kwa mujibu wa taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari nchini humo, almasi hiyo yenye uzito wa karati 709 imehifadhiwa kwenye benki kuu katika mji mkuu wa Free Town.

Almasi hiyo ni miongoni mwa almasi 20 kubwa zaidi kuwahi kupatikana. Wachimba migodi wa kujitegemea ni wengi kwenye migodi yenye almasi nyingi nchini humo.

Lakini kuna maswali ikiwa kama jamii itanufaika kutokana na kupatikana kwa almasi hiyo.

Almasi hiyo iliyogunduliwa ambayo thamani yake bado haijatangazwa ndiyo ya pili kwa kubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini Sierra Leone, tangu mwaka 1972 wakati almasi nyingi ya karati 969 ilipatikana.

Kwanza ilipelekwa kwa Rais Ernest Bai Koroma siku ya Jumatano kabla ya kupelekwa Benki Kuu.

Koroma alisema kuwa mmiliki wa almasi hiyo atapata haki yake na itainufaisha nchi. Sierra Leone ni maarufu katika biashara ya madini ya almasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles