30.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mchujo watumishi hewa kuanza leo

simbaaJOHANES RESPICHIUS NA FLORIAN MASINDE, DAR ES SALAAM

TAARIFA za watumishi hewa kutoka taasisi mbalimbali za umma, zinatarajiwa kuanza kuchambuliwa, kwa ajili ya kuandaa ripoti itakayowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli.

Hatua hiyo, imekuja baada ya kumalizika kwa siku 15 za agizo la Rais Dk. Magufuli kwa wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri la kuwataka kuhakiki watumishi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mshahara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),George Simbachawene  alisema tayari taarifa hizo zimewasilishwa wizarani kwa ajili ya kuzichambua na kuandaa ripoti moja itakayopelekwa kwa Rais.

“Karibu mikoa yote imewasilisha taarifa za watumishi hewa, kuanzia kesho (leo) tutakaa ili kuichambua na kuandaa ripoti moja.

“Watumishi hewa katika taasisi mbalimbali za Serikali wapo wengi na watoro, unakuta mtumishi hachukui fedha, zinachukuliwa na wanagawana na walioko ofisini,” alisema.

Alisema baada ya kuchambuliwa na kuandaa ripoti moja watashirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angela Kairuki, kuangalia ripoti hiyo.

Katika hatua nyingine, waziri huyo alisema mabasi ya mwendo  kasi  (DART) yanatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya kutatua changamoto zikizokuwa zikiukabili mradi huo.

“Mradi huu ulikuwa na changamoto nyingi, zimepatiwa suluhisho, muda wowote unaweza kuanza na kwa sasa tumeanza majaribio ya magari mawili, tunatarajia kuongeza mengine,” alisema.

Alisema kesho atafanya ziara ya kukagua vituo vya mradi huo kwa ajili ya kuangalia jinsi yanavyofanya kazi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles