24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mchina aliyeleta heka heka ya virusi vya corona achunguzwa

Aveline Kitomary -Dar es salaam

WIZARA ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha tetesi za kuwepo kwa mtu anayeshukiwa  kuwa na ugonjwa wa virusi vya corona nchini. 

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo –Idara kuu ya Afya, Catherine Sungura alisema kuwa  timu ya wataalamu wa afya ilifika eneo aliko mshukiwa huyo aliyetokea nchini China Februari 2 mwaka huu na kuingia jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo  baada ya kufanikiwa kumfanyia uchunguzi wataalamu hao walibaini kuwa raia huyo mwenye asili ya China  hana dalili za kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Aidha Wizara hiyo ilitoa rai kwa wananchi  kutokuwanyanyapaa raia wa kigeni hasa raia wenye asili ya China pamoja na watu wanaovaa ‘mask’ kwa nia ya kujikinga njia ya hewa  kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida duniani  ambao hutumika kwenye msongamano wa watu.

 “Pamoja na hayo Wizara imeimarisha ukaguzi wa afya mipakani na katika viwanja vya ndege kwa kuhakiksha watu wote wanaotoka na kuingia wanakaguliwa kikamilifu,” inasomeka taarifa hiyo.

Mlipuko wa virusi vya corona ulioanzia katika jiji la Wuhan nchini China mbali na kusababisha vifo vya watu 637  na maambukizi kwa watu 31,198 umesababisha hofu kubwa duniani.

Ugonjwa huo unaambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingia na majimaji yenye virusi kutoka kwa mtu mmoja kwa kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa na mafua makali, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, kuathiri mapafu, kupumua kwa shida na hadi kifo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles