26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mchepuko wakimbia nyumba kimya kimya baada ya kuzaa mtoto wa kike’

Na Oliver Oswald, Mtanzania Digital

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Khadija Mshamu, mkazi wa Tandika sokoni jijini Dar es Salaam, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumkimbia mume wa mtu aliyekuwa akiishi naye kwa muda wa miezi kadhaa katika nyumba aliyokuwa amepangishiwa katika eneo hilo.

Wakizungumza na Mtanzania Digital leo Februari 3, 2023 baada ya kutokea kwa kisanga hicho, baadhi ya wapangaji wenza na Khadija, walisema chanzo cha kuondoka kwa mpangaji huyo ni kukwepa aibu baada ya kujifungua mtoto wa kike tofauti na matarajio yake kwa mumewe ambaye ni mchepuko wake.

“Usiku wa kuamkia mwaka mpya mwenzetu aliondoka kimya kimya bila kuaga huku akiwa amebeba mkoba wake na mtoto mchanga ambaye alikuwa amejifungua siku chache zilizopita .

“Lakini cha kushangaza alivyo ondoka hadi leo hii tunavyo zungumza na wewe mwenzetu hajarudi na vitu vyake vyote kuanzia vyombo na kitanda bado vipo ndani.

“Sababu kubwa iliyo sababisha asirudi ni aibu ya kujifungua mtoto wa kike, kwani huyo mwanaume aliyekuja kumpangia hapa tegemeo lake ni kupata mtoto wa kiume kwani mkewe wa kwanza alikuwa na watoto wanne wote wa kike,” amesema mama Amina ambaye ni mmoja wa wapangaji katika nyumba hiyo.

Alisema, Khadija alihamia katika nyumba hiyo akiwa na mimba changa huku ‘mchepuko’ uliompangishia hapo ukiwa na tumaini la kupata mtoto wa kiume kwa kile kilicho sadikika kwamba Mkewe wa ndoa hakubarikiwa kupata mtoto wa jinsia hiyo kwa wakati huo.

“Kwa taarifa tulizo zisikia ni kwamba, huyu mwanaume alianza kumsaliti mkewe na kumtafuta mchepuko ili amzalie mtoto wa kiume, lakini kwa bahati mbaya baada ya kujifungua mchepuko alipata mtoto wa kike na kusababisha tahamaki kubwa kwa bwana huyo.

“Lakini baada ya wiki moja tukasikia mke mkubwa naye kajifungua mtoto wa kiume, kumbe naye alikuwa ni mjamzito,” amesema.

Alisema, baada ya mchepuko kusikia mke mkubwa amejifungua mtoto wa kiume alianza kukosa amani kwani hata huduma alizokuwa akipewa awali na mwanaume huyo hakuzipata tena.

Akizungumzia hali hiyo kwa njia ya simu , mume wa mchepuko huo ambaye hakutaka jina lake liandikwe mtandaoni , alisema ni kweli alimpangia Khadija katika nyumba hiyo kwa lengo la kumzalia mtoto wa kiume lakini bahati mbaya akajifungua jinsia ya kike ambayo hakuhitaji.

“Mimi kweli nilimpangia hapo ila hali ikaenda tofauti na makubaliano yetu kwamba yeye alisema anauwezo wa kunizalia ‘dume’ ndomana nilikuwa ninamhudumia kwa kila kitu nikitegemea hali itakuwa kama tulivyo panga.

Baada ya mambo kwenda tofauti nikaishiwa nguvu ya kuendelea naye kwani nilicho kitaka sijapata na kwakuwa hata mke wangu mkubwa alikuwa mjamzito basi nikasubiri nione atajifungua jinsia gani , lakini Nashukuru Mungu amesikia kilio changu amenipatia mtoto wa kiume niliyekuwa nikimtaka.

Kufuatia tukio hilo , mwanaume huyo amewaomba wanaume wenzie kuwa wavumilivu na ndoa zao pale wake zao wanapobarikiwa watoto wa jinsia moja kwani siku zote mpangaji ni Mungu.

“Numejifunza kitu kikubwa kwamba Mungu hapangiwi, nawaomba wanaume wenzangu tuwe wavumilivu na wake zetu endapo itatokea jambo kama hili kwenye ndoa zenu.

” Kuhusu vitu vilivyo telekezwa na mchepuko ntavifata maana vyote nilinunua kwa pesa yangu na endapo atantafuta mwenyewe kwa ajili ya huduma ya mtoto nipo tayali kumpa ushirikiano wote katika malezi kwani watoto wote ni sawa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles