30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mchengerwa aagiza kuwachunguzwa viongozi, wanufaika feki wa Tasaf

Na, Anna Ruhasha Sengerema

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa, ameiagiza Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU ), kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria walengwa walioigizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini ambao hawana sifa pamoja na viongozi walioshiriki kuwaigiza

Mchengerwa amesema hayo wilayani Sengerema mkoani Mwanza, katika ziara ya kikazi ya siku moja na kufanikiwa kuzungumza na baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf) katika Kata ya Nyamatongo na Katunguru zilizopo ndani ya wilaya hiyo.

Mchengerwa , amesema Serikali imetenga trioni 2.3 kwa ajili ya kuzifikia Kaya masikini nchi nzima kupitia mpango wa Tasaf awamu ya tatu mzunguko wa pili.

‘’ Niwaambieni Mheshimiwa Rais ametenga fedha nyingi kuhakikisha tunaenda kuzishika mkono kaya masikini zote nchi nzima bila kuziacha zenye sifa , naagiza mpitie upya takwimu , mkuu wa mkoa uko hapa , mkuu wa wilaya uko hapa.

“Pia TAKUKURU Tanzania nzima fanyeni uchunguzi mjilizishe kama kunakaya aipaswi kuwa miongoni mwa Kaya masikini. Kuna viongozi wamechomeka watu kupitia jina moja moja ili tuweze kujilidhisha, wakamatwe na viongozi waliousika pia,’’ amesema Waziri.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga, amesema katika zozezi la utambuzi wa Kaya masikini lililoanza mwanzo mwa mwaka huu wilaya yake imeogeza vijiji 51 ambavyo havikuwa katika mpango .

‘’Waziri zoezi la utambuzi limefanyika mwanzoni mwa mwaka huu katika vijiji , na mitaa 51 vilikuwa havijaingizwa kwenye mapango , katika utambuzi mpya tumeviingiza kwa wilaya nzima ambayo ina halmshauri mbili Buchosa na Sengerema, Buchosa tunawalengwa 1,779 na Sengerema 5,131 jumla waliopo kwenye mapango ni walengwa 6,910,”amesema Ngaga.

Baadhi ya wanachi waliojitokeza katika ziara hiyo

Naye Diwani wa Kata ya Nyamatongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Sengerema, Yanga Makaga amesema katika kata yake tangu mpango huo umeanza kutekelezwa mwaka 2014 , Kata ya Nyamatongo kati ya vijiji vinne kijiji kimoja cha Kalumo ndicho kilikuwa kwenye mpago .

‘’ Kwa mwaka huu vijiji vyote vimeigizwa kwenye mpango , kijiji cha Kabusuli, Kamaga na Nyamatongo , kati walengwa 447 wametambuliwa lakini katika utambuzi huo kaya nyingi zimeachwa ambazo zinasitahili kuigizwa katika mpango kwa hiyo tukuombe useme neno kwa kaya zilizoachwa ziweze kutambuliwa,“ amesema Yanga.
Wakati huo huo Mbunge wa jimbo hilo Hamis Tabasamu ,ameiomba serikali irudie zoezi lautambuzi nchi nzima kutokana na changamoto zilizopo za kuacha walengwa wengi wenye sifa katika maeneo yao .

‘’Mheshimiwa Waziri hawa unao waona ndiyo wapiga kura za Chama Cha Mapinduzi za uhakika, nimebeba nafasi yao nakuja kuomba katika hawa wazee zaidi ya 600 ni kijiji kimoja waliondikishwa Tasaf, sasa tunakuomba kama ni mabadiliko basi yaandaliwe nchi nzima ikiwemo upendeleo Sengerema na safari hii na mimi Mbunge nitalisimamia ‘’amesema Tabasamu.

Aidha amezungumzia suala la malipo kwa njia ya miamala ya simu kwa walengwa hao kuwa njia hiyo imekuwa changamoto kwao kutokana na asilimia 90 ya wazee mkoani Mwanza kutojua kusoma na kuandika hivyo baadhi yao kushindwa kubaini miamala wakati wa malipo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles