24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Mchekeshaji ategemewa kuwa rais Ukraine

KIEV,Ukraine

RAIA wa nchi hii jana  walimiminika vituoni  kwa ajili ya awamu ya pili ya uchaguzi usio wa kawaida, ambako mchekeshaji kwenye vipindi vya televisheni alitarajiwa kushinda.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha  a Volodymyr Zelensky mwenye umri wa miaka 41 atamshinda Rais wa sasa, Petro Poroshenko, huku kukiwa na hasira ya wapiga kura dhidi ya umasikini na ufisadi.

Vituo vya kura vilifunguliwa saa 11 alfajiri na kufungwa saa 11 jioni, na matokeo ya awali yalitarajiwa kujulikana saa kadhaa baadaye.

 Ushindi wa Zelensky utafungua ukurasa mpya wa historia ya nchi hii ambayo imekumbwa na mapinduzi ya umma mara mbili ndani ya miongo miwili na inakabiliwa na vita vya waasi wanaotaka kujitenga tangu mwaka 2014.

Ukraine inategemea misaada ya  mataifa na nishati kutoka Urusi, na rais ajaye wa taifa hili atapaswa kukabiliana na Rais Vladimir Putin wa Urusi na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles