24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mchekeshaji ashinda urais Ukraine

KIEV, Ukraine

MCHEKESHAJI   wa vipindi vya televisheni nchini hapa, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais  kutokana na kura zilizopigwa juzi.

Kura hizo zimempa nafasi mwanasiasa mpya ambaye amechaguliwa kwa kuungwa mkono na zaidi ya asilimia 70.

 Kwa ushindi huo, Zelensky mwenye umri wa miaka 41, ameweza kumtoa madarakani Rais Petro Poroshenko ambaye amekubali kushindwa.

Matokeo ya sasa yanaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa  Poroshenko na kukataliwa kuanzishwa kwa Ukraine mpya.

“Sitawaangusha ,”  Zelensky aliwaambia waliomuunga mkono wakati wa sherehe za kujipongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles