28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mchange akana tuhuma za mauaji ya Dk. Slaa

Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Habibu Mchange
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Habibu Mchange

GRACE SHITUNDU NA RAPHAEL NOLESCUS (TUDARCO)

ALIYEKUWA kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Habibu Mchange, ameibuka na kuponda hoja za kumuhusisha kupanga njama za kutaka kumuua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Alisema tuhuma hizo ni upuuzi na ni dalili ya kifo kwa chama hicho.

Hatua hiyo ya Mchange imekuja siku chache baada ya madiwani wawili wa Chadema Mkoa wa Shinyanga waliokuwa CCM, kuibua tuhuma hizo na kudai walitumwa ili walipue  ‘Chopa’ iliyokuwa imewabeba viongozi wa chama hicho akiwemo Dk. Slaa.

Diwani wa Kata ya Ngokolo, Sebastian Mzuka na Zakaria Mfuko wa Kata ya Masekelo, walidai kulikuwa na njama za kumuua Dk. Slaa zikipangwa na kile walichodai mtandao mpana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake kwa kutumia njia ya kulipua helkopta aliyokuwa amepanda katibu huyo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, John Mnyika.

Lakini Mchange alisema tuhuma hizo ni upuuzi ulioratibiwa na Tundu Lissu, ambao unathibitisha kushindwa na kuporomoka kisiasa kwa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mchange alisema katu hausiki na mpango huo, ila kuna mkakati wa Chadema kuhamisha ajenda kwa Watanzania.

“Haiingii akilini hata kidogo kwamba mimi Mchange nimepanga na CCM na naibu waziri kuilipua helkopta ambayo iliwabeba Slaa na Mnyika, kwangu mimi Slaa ni mwanasiasa dhaifu ambaye wala sihitaji kumfanyia hayo,” alisema.

Mchange alitolea mfano baadhi ya matukio yaliyofanywa na Chadema kuwa ni pamoja na lile la Arusha, Morogoro, Igunga, Shinyanga na Iringa ambalo Daud Mwangosi alipoteza maisha.

“Katika matukio hayo yote, Mbowe na Slaa wamekuwa wakimtumia kijana mmoja mrefu mweupe mwenye mazoea ya kufuga nywele nyingi, aliyechanganya uraia wa Tanzania na Ujerumani au nchi nyingine ya Ulaya, sitamtaja jina ila Mbowe na Chadema wanamfahamu.

“Kijana huyo ambaye kwa sasa ni kiongozi katika ngazi ya wilaya katika mkoa mmoja wa Kaskazini amekuwa akitumika kutekeleza mpango wa mauaji kwenye matukio makubwa ya mikutano ya kisiasa, hasa inayohusisha vurugu kati ya Chadema na polisi na kumuandaa mtu mmoja maalumu kwa ajili ya kupiga picha matukio hayo na kusambaza haraka mitandaoni huku mwingine akichukua video,” alisema Mchange.

Akizungumza na MTANZANIA, Mkurugezi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Chadema, Mnyika, alimtaka Mchange kujibu hoja za tuhuma na sio kuleta propaganda kwa kubadilisha mada.

“Hayo anayozungumza huyo Mchange ni propaganda, asikwepe kujibu mada bali ajibu kama si kweli yeye pamoja na viongozi wa CCM waliwanunua madiwani wale wa Chadema, lakini kutokana na kuwatapeli waliamua kurudi,” alisema Mnyika.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. kweli mnyika sasa wewe unaambiwa ulitumika kuwanunua madiwani wao ndio wanaosema unatakiwa kudhibitisha au kukana lakini unabadili mada hapo sio sawa katika tukio la mwangosi naona hapo umekosea kabisa maana hata video zinaonyesha ni nani aliyehusika na tukio hilo hapo unajikanyaga dogo. siasa hazipo hivyo na kwa taarifa yako hakuna atakaye kuunga mkono katika hoja dhaifu kama hiyo. inaonekana wewe siasa hujui ila ulikurupuka kujiingiza kwenye siasa mara baada ya kukosa ajira.

    na ukumbuke kuwa katika hili unapokuwa unaongea kitu watu wenye akili wanakuelewa mojakwa moja kwamba hoja zako ni dhaifu sanaa, hakuna mtu yeyeote atakaye kuunga mkono, hii yote inatokana na ukosefu wa kazi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles