25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mchakato wa mashtaka dhidi ya Trump waendelea

Washington, Marekeni

MCHAKATO wa mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump wa Marekani unaendelea katika Baraza la Seneti mjini Washington, kwa kusikiliza hoja za upande wa chama cha upinzani cha Democratic.

Kiongozi wa mashtaka upande wa chama hicho, Adam Schiff, alisema Trump alitumia vibaya madaraka ya ofisi yake kwa madhumuni ya kujiongezea nafasi ya kuchaguliwa tena.

Wademokrat wanamshutumu Trump kumshinikiza Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy kuanzisha uchunguzi dhidi ya makamu rais wa zamani, Joe Biden, ambaye anaweza kuwa mpinzani wa Trump katika uchaguzi wa urais wa Novemba.

Walisema alitumia msaada wa kijeshi unaotolewa na Marekani kwa Ukraine wa kiasi cha Dola milioni 391, kama chambo cha kuyatimiza malengo yake ya kisiasa.

Warepublikan ambao wanalidhibiti Baraza la Seneti, wanaendelea kuonyesha mshikamano na Rais Trump.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles