23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

MCHAKATO KUONDOA SHEHENA BANDARINI, MIPAKANI WAANZA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Serikali imeanza maadalizi ya kutengeneza mfumo wa pamoja wa kielektroniki wa uondoshaji shehena bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na mipakani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.

Akizungumza leo Jumatano Machi 28, Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau mbalimbali wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mfumo huo.

“Uwepo wenu katika mkutano huu ni muhimu sana kwasababu mtaweza kupitia mahitaji yote ya mfumo yaliyoandaliwa na watalaamu wetu ikiwa ni pamoja na maeneo ya kisheria, kiufundi na kibiashara ili muweze kuuboresha zaidi”, amesema Kichere.

Amesema serikali imelenga kuwawezesha wadau wote wanaohusika na biashara za kimataifa na usafirishaji wa mizigo kutumia Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena kwa lengo la kuwezesha uwasilishaji wa nyaraka mahali pamoja ili wadau wote waweze kushughulikia nyaraka hizo kwa wakati.

Naye Mratibu wa Mfumo wa Uondoshaji Shehena kutoka TRA, Felix Tinka amezitaja faida za mfumo huo kuwa ni pamoja na kurahisisha na kuwezesha biashara, kuongeza ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali na kuongeza uhiari wa ulipaji ushuru na tozo mbalimbali kwa waingizaji na waondoshaji wa mizigo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles