27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MCGREGOR ATUMA BARUA YA WAZI KWA MASHABIKI

LONDON, ENGLAND

BINGWA wa ngumi mchanganyiko nchini Ireland, Conor McGregor, ametuma barua ya wazi kwa mashabiki wake ikiwa ni siku chache baada ya kupokea kichapo kutoka kwa mpinzani wake, Floyd Mayweather.

McGregor alichezea kichapo hicho katika raundi ya 10, ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza mchezo huo wa ngumi kutumia mikono tupu, huku akiwa amezoea kucheza mchezo wa mateke na ngumi kwa wakati mmoja (UFC).

McGregor mwenye umri wa miaka 29, alipoteza pambano hilo mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ulingo wa T-Mobile Arena, jijini Las Vegas, dhidi ya bingwa Mayweather mwenye umri wa miaka 40.

Bingwa huyo wa ngumi mchanganyiko, McGregor, amewashukuru mashabiki na viongozi wake kutokana na kumpa nguvu ya kufanya vizuri, lakini amedai alishindwa kutokana na kukosa uzoefu.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru mashabiki wote walionisapoti katika pambano langu, ninaamini bila yenu siwezi kufanya lolote, hivyo sina budi kutoa shukrani za dhati kwenu. Napenda kuwashukuru timu ya makocha walionisimamia kwa kipindi chote cha maandalizi.

“Ninaamini nilikuwa na uongozi sahihi, haikuwa kazi rahisi kufika raundi ya 10 kati ya 12, hata hivyo wakati nipo mazoezini kila siku nilikuwa napambana kuhakikisha ninamaliza raundi ya 12, lakini bado kulikuwa na changamoto.

“Katika maisha yangu sijawahi kupigana zaidi ya dakika 25, lakini kwenye pambano hilo dhidi ya Mayweather niliweza kufika hadi dakika ya 30, ninashukuru nimeweka historia na nimejiongezea uzoefu.

“Hata hivyo, natakiwa kumpongeza mpinzani wangu, Mayweather kwa kuonesha uwezo wake, ni wazi kwamba uzoefu wake umemsaidia kwa kiasi kikubwa, namtakia kila la heri katika maamuzi yake ya kustaafu mchezo huo, ameweza kufanya kila kitu ambacho alikuwa anakitaka katika ngumi, hivyo ni sahihi kustaafu,” aliandika McGregor.

Mayweather tayari ametangaza kustaafu ngumi baada ya kucheza jumla ya mapambano 50 ya kulipwa na kushinda yote, kati ya hayo mapambano 27 ameshinda kwa KO. Baada ya kushinda kwa pambano dhidi ya McGregor, alitumia kiasi cha bilioni 4 kwa ajili ya kusherehekea ushindi huo, huku akiwa amechukua zaidi ya bilioni 650.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles