27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MBWA WAMUUA MTOTO WA RAIS MTEULE GAMBIA

BANJUL, GAMBIA


Adama BarrowMTOTO mwenye umri wa miaka minane wa Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow, amefariki dunia baada ya kung’atwa na mbwa.

Barrow, aliye nchini Senegal, anatarajia kuapishwa kesho, lakini Rais Yahya Jammeh ametangaza kwamba hataondoka madarakani.

“Mwana wa Rais mteule Barrow (51), Habibou, alifariki dunia jana (Jumapili) baada ya kuumwa na mbwa kadhaa,” kilisema chanzo cha habari cha kifamilia Jumatatu wiki hii.

Habibou, ambaye alikuwa mmoja wa watoto watano wa Barrow alizikwa Jumatatu jioni kwenye makaburi ya Kanifing, kitongoji cha mji mkuu wa Banjul na kushuhudiwa na waombolezaji kadhaa.

Hakuna maelezo zaidi kutoka kwa Barrow au ujumbe wake kuhusu mazingira ya kifo hicho.

Taifa hilo dogo la Afrika Magharibi limekumbwa na mgogoro wa kisiasa tangu Jammeh alipopinga ushindi wa Barrow Desemba mwaka jana na kukataa kuondoka madarakani.

Viongozi wa nchi jirani za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), mara kwa mara wamekuwa wakimtaka mtawala huyo wa muda mrefu kuondoka madarakani kwa amani bila mafanikio.

Msemaji wa Barrow alisisitiza rais huyo mteule kuapishwa kesho kama ilivyopangwa na yupo Senegal, alikowasili mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuhudhuria mkutano wa Afrika mjini Bamako, Mali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles