25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunifu Rehmtullah kuinua tasnia ya mitindo nchini

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mbunifu wa mavazi, Ally Rehmtullah ameweka wazi kuinua soko la mitindo nchini kwa kutoa mafunzo kwa wabunifu kuweza kutimiza ndoto zao na kujipatia kipato kupitia sanaa wanaoifanya.

Amesema kuwa takribani wabunifu sita wamehitimu katika darasa la ubunifu 101 ya mbunifuhuyo mkongwe.

Akizungumza jana wakati wa jukwaa kuhitimisha awamu ya kwanza ya mafunzo ya ubunifu lililoandaliwa na mbunifu huyo katika ukumbi wa The Drum jijini Dar es Salaam, Rehmtulla amesema lengo ni kusaidia vijana ili waweze kujiajiri.

“Napenda kuwainua wabunifu chipukizi nimeamua rasmi kuendesha darasa ambalo linalenga kuwaimarisha wabunifu hao pamoja na kuwatambulisha kwenye sekta ya ubunifu wa mavazi.

“Ni darasa ambalo linachukua muda wa miezi mitatu, linakutanisha wabunifu wakongwe ambao lengo ni kuwaongezea ujuzi na uwezo ili kuwa wabunifu waliokamilika hivyo ndio maana unaweza kuona muunganiko huo wa wabunifu wakongwe wapo kwa ajili ya kukuza vipaji hivi vipya,”amesema Rehmtullah.

Aidha, Rehmtulah amesema pamoja na yote hayo changamoto ipo kwenye fedha ya kuendesha madarasa hayo na ndio maana ameanza na watu wachache kwanza.

“Kuna baadhi ya vitu vinakua vigumu kuwapatia wanafunzi kwa wakati kutokana na changamoto ya kifedha kwa kuwa nafanya mwenyewe,” amesema mbunifu huyo.

Pia amewapongza Baraza la Sanaa nchini (BASATA) kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa majukwaa ya mavazi na kutoa ruhusa kuonyesha mavazi mbalimbali.

“Mwanzo ilikua shida hasa kwa wabunifu kuonyesha au kupita jukwaa na mavazi kama ya usiku au ya ufukweni kutokana na mavazi hayo kuonekana ni nje ya maadili yetu, lakini kutoka na walezi hao kukubaliana na hilo imefanya hata wabunifu wetu kuongeza uwezo na jitihada za kutengeneza mavazi hayo,” amesema.

Kwa upande wake mbunifu, Anna Joseph ambae ni miongoni mwa waliopatiwa mafunzo hayo amesema kupitia darasa hilo imemfungulia milango mingi ikiwemo kujuana na watu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles