27.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

MBUNGE WA MONDULI AKANUSHA KUHAMIA CCM

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam        


Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (Chadema) amekanusha taarifa za kuhama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa za kuhama Chadema zilianza kusambaa leo katika baadhi ya mitandao ya kijamii huku Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akiandika katika ukurasa wake wa Twitter kumtakia safari njema huko aendako akimaanisha CCM.

Kalanga anadaiwa kuwaaga baadhi ya viongozi wa Chadema ambapo pia alitarajiwa kutangaza uamuzi huo wa kujiunga na CCM kesho Jumanne Julai 31, jijini Arusha.

Hata hivyo, akizungumza na Mtanzania Digital kwa njia ya simu, Kalanga amesema hana mpango huo na kuongeza kuwa bado yupo sana Chadema.

“Huo ni uzushi tu, hata jana walisema Sumaye (Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati ya Chadema, Fredrick Sumaye) anaondoka leo, mbona bado yupo? ni uzushi tu, sina mpango huo,” amesema Kalanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles