25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge wa Makete ahoji zoezi la kuweka alama za mipaka

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Makete, Festo Sanga, amehoji ni lini Serikali itarudia zoezi la kuweka alama za mipaka kwa kuwashirikisha Wananchi ili kumaliza mgogoro uliopo wa mipaka kati ya Hifadhi ya Taifa Kitulo (TANAPA) na Wananchi wa Vijiji vya Misiwa, Makwalanga, Igofi na Nkondo.

Akiuliza swali leo Jumatatu  Februari 8, 2021, Bungeni Sanga alihoji ni lini Serikali itarudia zoezi la kuweka alama za mipaka kwa kuwashirikisha Wananchi ili kumaliza mgogoro uliopo wa mipaka kati ya Hifadhi ya Taifa Kitulo (TANAPA) na Wananchi wa Vijiji vya Misiwa, Makwalanga, Igofi na Nkondo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema serikali ilishaweka alama za mipaka za kati (intermediate beacons) kwenye maeneo ya Hifadhi ya Taifa Kitulo inayopakana na vijiji vya Misiwa, Mwakalanga, Igofi na mwaka 2018 katika Kijiji cha Nkondo. 

Naibu Waziri huyo amesema zoezi hilo la uwekaji wa alama lilishirikisha Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Makete, Waheshimiwa madiwani, Serikali za vijiji, wananchi kwa ngazi ya vijiji, pamoja na wataalam wa ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

“Elimu iliyotolewa kwa wananchi kuhusu zoezi la uwekaji alama za mipaka kwenye vijiji hivi kabla ya uwekaji wa alama za mipaka hiyo. Baada ya utoaji wa Elimu, wananchi walichagua wawakilishi watano katika kila kijiji ili kujiunga na timu ya watumishi kutoka Hifadhini.

“Na wataalam wa ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Makete, ili kufanya utambuzi wa eneo la mipaka na kuweka mipaka hiyo kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na.279 ya Mwaka 2005 ya uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa Kitulo,”amesema.

Amesema maeneo hayo tajwa yalikwisha wekewa alama za mipaka na zoezi hilo liliwashirikisha Wananchi kikamilifu.

Amesema Lengo kuu la zoezi hilo lilikuwa ni kuhakikisha kuwa mipaka inaonekana bayana, na pia shughuli za kibinadamu hazifanyiki ndani ya eneo la Hifadhi.

“Ni imani yetu kwamba mgogoro wa mipaka kati ya Hifadhi ya Taifa Kitulo na vijiji vilivyotajwa ulishapatiwa suluhu kwa kuzingatia Tangazo la Serikali, na tunachokiomba kutoka kwa wananchi ni ushirikiano wao ili kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles