28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Tabasamu aahidi kutatua changamoto ya Miundombinu Sengerema

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mbunge wa jimbo la Sengerema mkoani mwanza, Hamis Tabasamu amewahakikishia wananchi wa jimbo lake kuwa katika uongozi wake atahakikisha anaondoa changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara za mitaa ambazo zilikuwa hazipitiki kwa urahisi.

Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi wakati wa kukagua barabra ya Michigani kuelekea Twitange yenye urefu wa zaidi ya kilometer mbili, Tabasamu amesema wananchi wa Halmashauri ya Sengerema wameteseka kwa miaka mingi bila barabara hiyo kupitika kwa urahisi na kusababisha changamoto kwa watumiaji.

“Kwanza ni mshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kutupatia fedha nyingi za kutengeneza barabara za mitaa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022 hadi 2023 haijawai kutokea Sengerema ikawa barabara za viwango kama ilivyo sasa serikali ya awamu ya sita inayojali wananchi wake,”amesema Mbunge.

Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa kuna baadhi ya barabara zitatengenezwa kwa kiwango cha lami ikiwamo ile ya Kamanga Sengerema na Sengerema sekondari.

“Kwa maeneo ya mjini kuna barabara zimo kwenye mpango wa kutengezwa kwa kiwango cha lami, lakini pia niwaondoe wasiwasi wananchi wa Sengerema barabara za mitaa nitahakikisha zinapitika kwa mwaka mzima bila kero,” amesema Tabasamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles