21.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

MBUNGE RWEIKIZA AWAAHIDI DONGE NONO DARASA LA 7

Na Mwandishi Wetu


MBUNGE wa Bukoba Vijijini (CCM), Jasson Rweikiza, ameahidi kuwapa zawadi ya donge nono wahitimu wa darasa la saba wa Shule ya St. Anne Marie Academy ya Mbezi  watakaofanya vizuri kwenye mitihani yao.

Rweikiza ambaye pia ni mkurugenzi wa shule hiyo alitoa ahadi hiyo wakati wa mahafali ya shule ya msingi na awali yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi,   Dar es Salaam.

Alisema ana uhakika wa asilimia 100 kwamba wahitimu wanaotarajiwa kumaliza darasa  la saba mwaka huu wameandaliwa vizuri na pamoja na kufanya mahafali hayo atawaita wazazi kusherehekea ushindi wa vijana wao.

“Nawashukuru wazazi kwa ushirikiano wao na walimu na kujitahidi kulipa ada kwa wakati, binafsi ninafurahia kuona wazazi wanavyojitahidi kulipa ada kwa wakati.

“Kinachonifurahisha ni watoto wetu wameiva na nina uhakika wa asilimia 100 vijana hawa watafaulu,” alisema.

Wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo walipongeza uwekezaji mkubwa kwenye taaluma uliofanywa na uongozi wa shule hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Maria Kaswala, alisema wazazi wamefurahishwa na uwezo walioonyesha wanafunzi wa shule hiyo kuanzia shule ya awali na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano.

“Tumeshuhudia namna watoto wa shule ya watoto wadogo wanavyomudu kutoa maelezo kwa lugha ya kiingereza na hata nyimbo za kitaaluma walizoimba zinaonyesha kweli wameiva, walimu mnafanyakazi vizuri hongereni,” alisema.

Mzazi mwingine, Antony Gervas, alisema matokeo mazuri ya shule hiyo kuanzia msingi hadi sekondari yanawapa imani wazazi kufanyakazi kwa bidii kutafuta ada kulipa watoto wao.

Akizungumza kwenye mahafali hayo, Mkuu wa Shule hiyo, Gladius Ndyetabura, alisema kwenye mitihani ya moko ya kata  wanafunzi wote wa shule yake wamepata wastani wa alama A na wanafunzi 10 bora wametoka shule hiyo.

Alisema kwenye matokeo ya wilaya wanafunzi  wote wamepata wastani wa alama A na wanafunzi 10 bora  wa kike na 10 bora wa kiume wote wametoka shule hiyo.

Alisema shule hiyo imekuwa ya kwanza kati ya shule 120 Wilaya ya Ubungo na kutunukiwa cheti na mkurugenzi wa wilaya ya hiyo pamoja na wanafunzi watatu wa kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,813FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles