MBUNGE: MAKONDA ALICHEZEA VYEUPE AMEKUTANA NA CHEUSI KIMEMTIA DOA

0
1434

 
Mwandishi Wetu, DodomaMbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF), amemsifu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kwa ‘kuyang’ang’ania’ makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimtaka kuyalipia kodi.

Makontena hayo ambayo yaliingizwa Bandari ya Dar es Salaam kwa jina la mkuu huyo wa mkoa yakidaiwa kuwa na samani za walimu wa shule mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo yalitakiwa kulipiwa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yakitakiwa kulipiwa kodi suala lilioungwa mkono na Waziri Mpango na kuamuru yazuiliwe hadi yatakapolipiwa kodi na yasipolipiwa yapigwe mnada huku Rais John Magufuli akipigilia msumari wa mwisho kumtaka Makonda ayalipie kodi makontena hayo.

Akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Septemba 11, Haji amesema mawaziri wa aina ya Dk. Mpango ndiyo Rais Magufuli anaowataka.

“Mheshimiwa sheria ni msumeno na katika kutekeleza majukumu yako muhimu ya kusimamia fedha za nchi hii hutakiwi kumwangalia usoni yeyote anayevunja sheria za nchi hii katika kusimamia kodi za wananchi.

“Kwa hiyo kitendo chako kitabakia katika historia, alijaribu kuwachezea wengine lakini alichezea vyeupe amekutana na cheusi kimemtia doa, na nakuambia Dk. Mpangio uzi ni huo huo mbane Makonda hadi mwisho ili haki ipatikane,” amesema Khatibu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here