25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE CHADEMA: TRA ARUSHA INATESA WAFANYABIASHARA

Na Eliza Hombo, Dodoma


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema   Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuwa ikiwatesa na kuwasumbua wafanyabishara hasa katika miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya.

Lema alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akiuliza swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunafahamu jitihada za serikali ya awamu hii ya kupigania sera ya viwanda ambalo ni jambo jema.

“Kila mwenye akili timamu analipongeza ili suala la viwanda liwe na ukweli ni lazima wawekezaji na wafanyabiashara wawe na mazingira bora.

“TRA wamekuwa wakitesa na kusumbua wafanyabishara hasa katika miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya hasa katika  mkoa ninakotoka, TRA wanatumia polisi, Takukuru na usalama wa taifa kuwatishia katika masuala ya kodi.

“Ili waweze kufanya biashara zao kwa uhakika nini kauli ya serikali juu ya mfumo wa TRA?”alihoji Lema.

Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema ni kweli kipo chombo kinachowajibika kukusanya kodi kutoka kwa walipa kodi wakiwamo wafanyabishara.

“Ni kweli wanatambau ulipaji kodi ni wadaiwa sugu, TRA kupitia chombo chake Task Force makao makuu, ilikuwa na mkakati wa kuwapitia wadaiwa sugu. polisi, Takukuru walienda kule kuona hakuna utoaji rushwa.

“Na katika msafara huo kama Arusha, polisi walikuwa wanatumia silaha na utaratibu kama fedha zinaweza kulipwa papo kwa papo na nimshukuru RC wa Arusha kwa kuwaita wafanyabishara na kuwaeleza wale polisi walikuwapo kwa ajili ya kulinda tu na alirudisha amani.

“TRA inao utaratibu, wale ambao wanadhani haiwatendei haki kusikiliza kero watumie madawati hayo kupeleka malalamiko hayo.

“Serikali inawaheshimu wafanyabishara na inatambua umuhimu wao wa kulipa kodi na kila mmoja  atambue wajibu wetu na waendelee kutoa ushirikiano na haiwapelekei hofu,”alisema Majaliwa.

Katika swali la nyongeza  Lema aliuliza: ”Kwa sababu TRA ina sheria zake na kwa kuwa hiyo task force inahusu wadaiwa sugu, kwa nini sheria hizo zisitekelezwe kuliko kutumia hiki chombo task force ambacho kinatumia Takukuru, usalama wa taifa… kwa nini hata kama ni task force wasihusu TRA na sheria zote?”

Akijibu hilo, Majaliwa alisema: ”Kama ambavyo nimesema, task force ni kwa ajili ya watu ambao kwa makusudi hawataki kutekeleza kulipa kodi kwa kuwatembelea wachache si wote, malengo hapa kila mmoja ana wajibu wake, polisi kama kulipa hadi afuate ulinzi wa fedha.

“Takukuru yupo pale kulinda rushwa kila mmoja ana wajibu wake mdaiwa sugu kama hataki anapelekwa polisi.

“Hakuna vitendo vya vionevu na halilengi kumtisha mfanyabishara. Pamoja na haya yote yanayoendelea task force haina nia mbaya kabisa wawe na amani”. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles