NA KOKU DAVID
KIKUNDI cha Kwaya ya Redemption cha Kanisa la Pentekoste lililopo Tabata Kinyerezi jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita kimefanya uzinduzi wa albamu yake ya kwanza yenye nyimbo 10.
Katika uzinduzi huo uliofanyika kanisani hapo, mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu wa Wilaya ya Ilala kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Anatropia Theonest, ambaye alilichangia kanisa hilo Sh milioni moja kwa ajili ya kununua kinanda katika kanisa hilo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mbunge huyo alisema kanisa lina nafasi kubwa ya kuirekebisha Serikali pindi itakapokwenda kinyume na kumpendeza Mungu hivyo amewataka viongozi wa dini kuwashirikisha viongozi wa Serikali katika masuala mbalimbali ya kanisa.
“Naomba kanisa liwafundishe waumini wake ujasiriamali ili waweze kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha na waondokane na utegemezi wa kuomba misaada,” alisema Anatropia.