30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Chadema ataka kuzichapa bungeni

Mwita WaitaraNa Elizabeth Hombo, Dodoma

MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), ametolewa ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kutaka kumpiga mbunge mwenzake wa Kasulu Vijijini, Agustino Hole (CCM).

Tukio hilo lilitokea jana saa 12:07 jioni, wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria, ambapo mbunge huyo wa Kasulu Vijijini, alikuwa akirusha vijembe dhidi ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu.

Alisema: “Ninaamini maneno ya mtaani yanasemwa kuwa ndugu yangu Lissu ana faili pale Mirembe,” alisema akiwa anaendelea na mjadala wake ndipo alisimama Lissu na kuomba mwongozo wa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akitumia kanuni za Bunge na kumtaka mbunge huyo kuthibitisha kile alichokiita uongo dhidi yake.
“Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ninafahamu Mirembe ipo katika eneo moja, ipo hapa katika Mkoa wa Dodoma, sijawahi kufika na wala

sipajui. Kwa hali hiyo mzungumzaji athibitishe jambo hili kwani amesema uongo,” alisema Lissu.
Kutokana na hali hiyo, Dk.Tulia alimtaka mchangiaji, Hole kufuta kauli yake na alipopewa nafasi hiyo, aliendelea kujenga hoja ikiwamo kufuta kauli.

Hata hivyo, alipokuwa akiendelea kuchangia, mbunge huyo aliendelea kurusha vijembe ambapo akiwa anaendelea ndipo Waitara alimfuta jirani na kiti chake huku akimsogelea kwa lengo la
kutaka kumpiga, ndipo Naibu Spika Dk. Tulia, alimuona na kuamuru atolewe nje na askari wa Bunge.
Baada ya kutolewa kwa amri hiyo, askari wa Bunge aliingia na kumtoa Waitara, nje ya ukumbi wa Bunge.

VIJEMBE

Mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria jana ulitawaliwa na vijembe na mipasho, huku Naibu Spika, Dk. Tulia akiwatuliza na
kuwaonya wabunge waliokuwa wakitumia lugha za kuudhi.

Wakati akichangia, Mbunge wa Ulanga, Mashariki, Goodluck Mlinga (CCM), wakati wote alikuwa akitumia maneno ya kuudhi akisema ili mtu aingie

Chadema na awe mbunge wa viti maalumu lazima aitwe ‘baby’.
“Lissu ameshauri wasiingie kwenye uchaguzi, sasa CUF wanasema mwanasheria mcharuko kiasi hiki,” alisema.
Alisema: “Sina shaka na Lissu kuhusu sheria. Kuna mapenzi ya jinsi moja.”
Kutokana na hali hiyo naye aliombewa mwongozo, hata hivyo mbunge huyo
alifuta kauli yake na kuendelea na mjadala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles