26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE CHADEMA AFUTA KAULI KWA ‘MBINDE’, ADAI WATUMISHI WALIOHAMIA DODOMA HAWAJALIPWA

Mwandishi Wetu, Dodoma


Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema), amelazimika kufuta kauli yake ya kwamba watumishi wa serikali waliohamishiwa Dodoma, hawajalipwa stahili zao.

Mwambe alikuwa akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi ya mwaka 2018 leo Septemba 4, bungeni uliowasilishwa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo.

Akiendelea kuchangia mjadala huo, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisimama kumpa taarifa mbunge huyo ambapo alisema anazo taarifa za uhakika zenye uthibitisho kuwa wote wameshalipwa stahili zao kwa kuhamia Dodoma.

“Mheshjimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa taarifa mbunge kuwa taarifa anazochukua huko anakopata si za kweli wote wameshalipwa,” amesema Jenista.

Hata hivyo, Mwambe baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza tena alisema hapokei hiyo taarifa kwa sababu watu hao wanakutana nao mitaani na wanasema hayo.

Majibu hayo yalimuibua tena Waziri Jenista, ambaye alisema kwa kutumia Kanuni ya 64 (1), Kanuni ndogo b, mbunge hatatoa taarifa ambazo hazina ukweli.

“Mwenyekiti ninasoma pamoja na kanuni ya 63, ambayo inataka nitoe uthibitisho wa jambo ninalosema, mimi kama waziri ninao ushahidi wa kuhamia Dodoma kwa awamu zote nne watumishi wamelipwa, namuomba mbunge ama atoe uthibitisho au afute kauli yake,” amesema.

Hatua hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kusimama na kusema; “Mambo mengine huwa tunayakuza tu, waziri amelithibitishia bunge yeye ni kweli lazima atoe ukweli ambao yanalifanya bunge liamini, mimi ningelikuwa wewe ningeenda moja kwa moja kwamba watumishi wamelipwa stahiki zao, hiyo ndiyo njia nzuri ya kwenda mbele.”

Akijibu taarifa hiyo, Mwambe alisema: “nimefundishwa kusema ndiyo na hapana lakini anayetakiwa kuthibitisha ni yule ambaye anasema mimi nimesema uongo.”

Baada ya kauli hiyo, Chenge alisema; “nimejieleza nilikuwa namuongoza waziri atufikishe kwenye kanuni ya 63, si kwamba ajielezee, hatua inayofuata tutaangalia uthibitisho wa wafanyakazi waliokuja Dodoma, sasa tuambie unafuta kauli au utaleta uthibitisho?” alihoji Chenge.

Hata hivyo, Mwambe alisema anafuta kauli na kuongeza kuwa ukweli huu utaendelea kuishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles