22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mbunge CCM apokewa kwa vibatari

Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu (CCM)
Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu (CCM)

Na AMINA OMARI, MUHEZA

WANANCHI katika Kijiji cha Songa, wilayani Muheza, Mkoa wa Tanga, wamesimamisha msafara wa Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu (CCM), wakiwa na ndoo tupu vichwani pamoja na vibatari.

Tukio hilo lilitokea jana asubuhi na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanaasha Tumbo, aliyekuwa katika msafara huo.

Wananchi hao walibeba ndoo hizo kuonyesha kukerwa na uhaba wa maji unaowakabili na vibatari walivyobeba vilikuwa vikionyesha mahitaji ya umeme kijijini hapo.

Pamoja na kubeba vitu hivyo, pia walikuwa na mabango yaliyokuwa na maandishi yaliyosomeka, tumechoka na kero za ukosefu wa maji na umeme.

Wakati mbunge na mkuu huyo wa wilaya wakizuiwa, walikuwa wakitoka kuzindua kisima kirefu cha maji katika Kijiji cha  Kwamianga.

Kutokana na wingi wa watu waliokuwa barabarani mbunge huyo alilazimika kusimamisha msafara na kuanza
kuwasikiliza.

Akizungumza na wananchi hao, Rajabu alisema mradi aliokuwa akitoka kuuzindua awali ulipangwa katika Kijiji cha Songa, lakini ulihamishwa na kupelekwa kijijini Kwamianga baada ya wakazi wa Kijiji cha Songa kukataa kuuchangia fedha.

“Huo mradi ulikuwa wenu, lakini ulihamishwa kwenda Kwamianga kwa sababu mlikataa kuchangia shilingi milioni 2.5.

“Kwa hiyo, nawaomba muwe mnachangia miradi ya maendeleo kwani Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu kwa kuwa ina majukumu mengi,” alisema Rajabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles