22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge CCM akabidhi vitendea kazi kwa vijana

Mwandishi wetu -Dar es salaam

MBUNGE wa Viti Maalumu, Mariam Ditopile, amekabidhi vitendea kazi zikiwemo kompyuta zenye thamani ya Sh milioni mbili na fedha tasilimu Sh 600,000 kwa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Akikabidhi vifaa hivyo juzi katika kikao cha Baraza la Vijana, Ditopile aliwaasa UVCCM kujitokeza hadharani kujibu hoja ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa CCM na Serikali zake.

Pamoja na hilo, aliwataka vijana hao kuyaeneza mazuri ambayo yamekuwa yakifanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli bila kuwa na aibu.

“Niwasihi vijana wenzangu kuwa mstari wa mbele kuyasema na kuyatangaza hadharani yale yote yanayofanywa na Serikali ya CCM katika kutekeleza ilani yake ya mwaka 2015, ambao ndio msahafu unaotuongoza ndani ya miaka hii mitano.

“Na tunaposema tuunge mkono juhudi za Rais Magufuli katika hizi zama za kuchapa kazi kama kaulimbiu yake inavyosema ya hapa kazi tu, wananchi nao wajue ni kazi kweli kwa sababu hata sisi vijana tutaonekana kweli tunaitekeleza ilani kwa kufanya kazi,” alisema Ditopile.

Aidha aliwapongeza UVCCM Dar es Salaam kwa kuwa waasisi wa CCM ya Kijani ambayo sasa imeshika kasi nchi nzima kwa kuwazindua wanachama na viongozi wajibu wao kueleka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles