25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE CCM AELEZA NAMNA MAPATO YALIVYOSHUKA

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM)

 

 

Na MAREGESI PAUL-DODOMA

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), amesema kama Serikali haitabadilisha njia za kukusanya kodi, uwezekano wa nchi kupiga hatua ni mdogo kwa kuwa hazikusanywi ipasavyo.

Bashe aliyasema hayo bungeni jana alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2017/18, iliyowasilishwa juzi na Waziri Dk. Philip Mpango.

“Mlipa kodi mkubwa nchini ambaye ni TBL, ameshusha kodi yake kwa Sh bilioni 50 katika mwaka wa fedha 2016/17.

“Taarifa za Wizara ya Fedha nazo zinaonyesha ‘payee’ imeshuka, VAT kwa ‘import goods’ imeshuka na mapato ya bandari nayo yameshuka kwa asilimia 13. Katika haya, najiuliza maswali mengi, hivi hawa wataalamu wetu hapo wizarani wanafanya nini?

“Hadi wakati huu, biashara 7,700 zimeshafungwa, ajira nazo zimepotea, nazidi kujiuliza, ‘what is the bottom line’. Mheshimiwa mwenyekiti, tatizo letu hapa ni wingi wa kodi ingawa sisi hatuelewi. Serukamba amesema hapa jana, kwamba katika kila biashara binafsi, Serikali ni mbia kwa asilimia 30.

“Taarifa za Wizara ya Fedha zinaonyesha biashara laki mbili zimefunguliwa ingawa ‘impact’ ya kufunguliwa kwa biashara hiyo hatuioni kama tunavyoona ‘impact’ kwa biashara kufungwa.

“Dk. Mpango sina shaka na taaluma yako, nakuomba muwaite wafanyabiashara wakubwa kama TBL mzungumze nao kwa sababu siku zote kodi haikusanywi kutoka kwa watu masikini, bali inakusanywa kwa wafanyabiashara wakubwa.

“Nawaambia kabisa, sitavumilia kulisema hili kwa sababu kulitambua hakuhitaji kuwa na Phd au uprofesa,” alisema Bashe.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=MlfXa2m-WuA[/embedyt]

Pamoja na hayo, mbunge huyo alieleza jinsi Kampuni ya Cocacola Kwanza ilivyopunguza wafanyakazi 130 baada ya uzalishaji kushuka na kusema hiyo ni dalili ya hali ngumu inayowakabili wafanyabiashara nchini.

Pia, alisema baadhi ya wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi, wameanza kuitumia Bandari ya Mombasa, Kenya kwa kuwa kodi zimekuwa nyingi nchini.

Kwa mujibu wa Bashe, katika mwaka wa fedha 2014/15, asilimia 1.4 ya bidhaa zilizoingia nchini Kenya kupitia Bandari ya Mombasa, zilitakiwa kuingia Tanzania na mwaka wa fedha 2016/17, asilimia 2.2 ya bidhaa zilizoingia nchini humo zilitakiwa kupitia Tanzania.

Wakati Bashe akisema hayo, Mbunge wa Konde, Khatibu Haji (CUF), alisema Serikali inatakiwa ijiulize ni kwa nini Marekani imesitisha misaada yake kupitia Mfuko wa Changamoto ya Milenia (MCC) baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2015 na uwepo wa Sheria ya Makosa ya Mtandao.

“Lazima mjiulize kwa nini MCC wamesitisha misaada yao, ingawa tukisema hapa watu wengine mnanuna. Pia, nyie mawaziri mwambieni ukweli mheshimiwa rais, kwamba hali ya uchumi ni mbaya huko mitaani,” alisema Haji.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), aliitaka Serikali ibuni mbinu mpya za kukusanya kodi badala ya kuendelea kuwabana wafanyabiashara wadogo ambao wengi wao wameanza kufunga biashara.

Pia alisema Watanzania kwa sasa wana maisha magumu, huku akionekana kutoridhishwa na kauli ya Serikali inayosema uchumi unazidi kukua wakati wananchi wanazidi kuwa na maisha magumu.

Kwa mujibu wa Ridhiwani, uchumi bora lazima uendane na maisha bora waliyonayo wananchi.

Wakati huo huo, baadhi ya wabunge walilalamikia kitendo cha Serikali kushindwa kupeleka Sh milioni 50 katika kila kijiji kama ilivyoahidi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Kwa mujibu wa wabunge hao, hali hiyo itawafanya wananchi wakose imani na Serikali yao kwa kuwa wamekuwa wakiulizia fedha hizo mara kwa mara.

Waliozungumzia fedha hizo ni wabunge wa CCM, Sauli Amoni wa Rungwe na Frattey Masay wa Mbulu Vijijini.

Kwa upande wake, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), pamoja na kuipongeza Serikali kutokana na utendaji kazi wake, alizungumzia suala la mchanga wa madini uliozuiwa katika makontena na kusema uamuzi huo ni sahihi kwa sababu wawekezaji wa dhahabu walikuwa wakiiibia nchi.

“Mimi ni Mbunge wa Msalala ulipo Mgodi wa Bulyankulu. Kati ya mwaka 2008 hadi 2009, wananchi walikuwa wakivamia malori ya mchanga wa dhahabu na kuchukua mchanga na waliokuwa wakichukua mfuko wa kilo 50 na kuchenjua dhahabu kwa njia za kawaida, walikuwa wakiuza dhahabu na kupata Sh milioni 50.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles