23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge azindua Maendeleo Podcast

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia kundi la asasi za kiraia (NGO’s),Neema Lugangira,amezindua maudhui ya elimu kwa njia ya mtandao “Maendeleo Podcast” ambayo yatatumika kutoa  elimu katika nyanja mbalimbali.

Akizungumzia uzinduzi huo jana jijini Arusha,Neema amesema anaamini kupitia maudhui hayo ataweza kuwafikia watanzania wengi wataalamu na viongozi mbalimbali hapa nchini,wananchi watapatiwa elimu kupitia mada mbalimbali.

Ametaja miongoni mwa masuala yatakayokuwa yanajadiliwa ni pamoja na wanawake na siasa,lishe,uwajibikaji wa sekta ya azaki ili ziweze kufanya kazi kwa tija na kuchangia maendeleo endelevu kwa taifa,wanawake wanaojishughulisha katika sekta za mifugo,uvuvi na kilimo pamoja na ushiriki aa wanawake kwenye sekta ya uziduaji ikiwemo gesi asilia na madini na watoto wa kike.

“Kwa kufanya hivi itatoa fursa kwa wataalamu na viongozi kuelimisha jamii na pia ifasaidia katika kuimarisha uelewa wa maeneo mbalimbali ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele zaidi.

“Kama mbunge wa kwanza kuanzisha hili vipindi vyangu vitakuwa vinaruka mara mbili kwa mwezi,na nitakuwa naandaa mjadala kupitia mitandao ya kijamii na kuleta wataalamu na viongozi mbalimbali,”

“Mbali na wananchi kufahamu masuala ya  maendeleo kupitia maudhui hayo ya kimtandao kwa njia ya sauti,wananchi wataweza pia kuelewa kazi kubwa za maendeleo anazofanya Rais wetu Samia Suluhu Hassan,”amesema Neema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles