Mbunge atoa msaada Sh mil 20/-

0
699

NA ASHA BANI -DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Temeke,Abdallah Mtolea amekabidhi Sh  milioni 20 kwa kikundi cha Umoja wa Wanawake wenye Ulemavu Temeke(UWAVIUTE).

Mtolea, alisema fedha hizo zimetolewa na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), baada maombi ambayo waliwasilisha katika kampuni hiyo kutokana na umuhimu na changamoto za kikundi hicho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mtolea aliishukuru kampuni hiyo kwa mchango wao wa kuijali jamii, huku akiomba mashirika mengine yawe na moyo wa kutoa kwa kuijali jamii yenye uhitaji maalum.

Alisema fedha hizo, zitasaidia kununua cherehani,kulipia pango na mahitaji mengine ya kina mama hao kama ambavyo waliomba.

“Ulemavu sio udhaifu ni watu ambao wanatakiwa kujikita katika futsa mbalimbali, tunatakiwa kuwafanyia wepesi kuwapa fursa mbalimbali na sio kuwabagua.

“Kuna kazi kwa mfano za mapokezi, kufungua tu kizuizi kwenye geti kwa ajili ya kuruhusu magari kuingia katika ofisi na kutoka hizo ni za kawaida, tunaweza kuwapa kwa sababu ni za kukaa muda wote na wao wakapata ridhiki,”alisema Mtolea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here