27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge ataka wakulima na wafugaji kuondoa tofauti zao

Mohamed Hamad

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian (CCM), amewataka wakulima na wafugaji kuheshimiana ili waweze kuendesha maisha yao.

Wakulima na wafugaji maeneo ya Kiteto wamekuwa wakigombea ardhi na kusababisha madhara yakiwemo kujeruhiana na kusababisha uharibifu wa mali.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Matui, Ndirigishi, Loolera, Bwagamoyo jana alisema kuna migogoro kila Kijiji na kuzitaka pande hizo kuondoa tofauti zao.

“Kuna tatizo Kiteto ambalo linachafua taswira ya Wilaya, kitendo cha wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima hilo sio sawasawa” alisema.

“Wilaya ya Mbulu ina mifugo mingi sana lakini hauwezi kusikia migogoro ya ardhi, na maeneo mengine, sasa nahitaji tuache kulisha mashamba na tuheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi,” alisema.

Aidha amewataka kuheshimu maeneo ya kilimo na maeneo ya wafugaji yasivamiwe ambapo amesema hayo yatafanikiwe endapo pande hizo zitaheshimiana na kufuata mpango wa matumizi bora ya ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles