26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge ataka vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume vipigiwe kelele

Na Safina Sarwatt,Mwanga

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kilimanjaro, Esther Maleko amewataka wanawake nchini kupaza sauti katika kupinga vitendo vya kikatili na ulawiti kwa watoto wa kiume, vinavyoendekea kufanywa na baadhi ya watu katika maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu

Maleko ameyasema hayo Februari 22,2023 wilayani Mwanga wakati alipotembelea vikundi vya akina mama wa UWT vinavyohusisha na shughuli za ujasiriamali.

Amesema Serikali ya awamu sita chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan imekuwa kipaumbele katika kuhakikisha inawezesha wanawake kiuchumi ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Amesema kuwa mwanamke wakiwezeshwa kiuchumi hata vitendo hivyo vya ukatili vitapungua kutokana na kwamba watakuwa karibu na watoto wao.

“Wamama msikubali hakikisheni tunaungana kwa pamoja kuupinga ukatili huu ambao wanafanyiwa watoto wetu wa kuime huko majumbani na baadhi ya wazazi na mashuleni hili siyo jambo la kulifumbia macho, tuwe na kauli moja tusema sasa basi ya tosh,” amesema Maleko.

Amesema tatizo hilo likiachwa likaendelea litaathiri nguvu kazi ya taifa na kukosekana viongozi bora wa baadae.

Katika zaira yake Maleko alikutana na kikundi cha wakina mama Maghariba walikuwa wakijihusisha vitendo vya ukeketaji ambapo kwa sasa wameachana na shughuli hizo baada kupatiwa elimu na kufunguliwa mradi wa utegenezaji wa majiko banifu ili kujipatie kipato.

Nao baadhi ya Mangariba hao wamesema wameachana na shughuli za ukeketaji baada ya kuelemishwa kuhusu madhara ya ukeketaji na kuwezeshwa kiuchumi kwani walikuwa wakitumia shughuli hizo kujipatia kipato cha kuhudumia familia zao ambapo wa siku walikuwa wakipata 20,000 hadi 30,000.

Sauda Msangi amesema kuwa kwasasa wameachana na shughuli za ukeketaji na kwamba wamejikita katika shughuli za ujasiriamali mali na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.

Katika ziara yake Maleko ametembelea kikundi cha wanawake cha Jikomboe kinachojihusisha na shughuli za fyatua matofali kilichopo Mgagao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles