22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

MBUNGE ATAKA SERIKALI KUUZA NDEGE KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

Gabriel Mushi, Dodoma

Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara (Bwege), ameitaka serikali kuuza moja ya ndege zake za Bombardier zilizonunuliwa ili kutatua tatizo la maji nchini.

Pia amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kuongoza zoezi la kupiga kura ili wabunge waamue kipaumbele iwapo wanahitaji maji au ndege.

Bwege ametoa kauli hiyo leo wakati akichangija bajeti ya wizara ya maji na umwagiliaji ambapo pamoja na mambo mengine amesema tatizo si mawaziri mizigo bali ni serikali.

“Kama hakuna maji hadi 2020, CCM kwa heri kwa sababu  magereza hakuna maji, lazima tutie udhu tupate maji naomba sana spika tuuze ndege tutatue tatizo la maji. Kwa kuwa uko vizuri leo piga kura wanaotaka ndege na maji tuone.

“Nilisema siku moja wakati huo rais akiwa waziri, nilimwambia wewe sio mzigo, mzigo ni serikali ya CCM kwa sababu leo tunasema asilimia 22 pekee ya fedha za miradi ya maendeleo ndiyo zimetoka, sasa afanye nini waziri wakati hajapata asilimia 78.

“Hivi leo mwananchi umuulize ndege na maji, kweli ninyi wabunge mnaoonea wananchi huruma tukiwaulizeni, kununua ndege na kuwapa watu maji, bora nini?” amehoji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles