28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge ataka REA iunde tume maalumu kusimamia miradi ya umeme

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema), ameitaka Wizara ya Nishati kuunda kitengo maalumu cha kusimamia miradi ya umeme ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Mei 29 bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2019/20 ambapo amesema kumekuwa na changamoto katika usimamizi wa miradi ya Rea.  

“Mradi wa Rea mnachelewesha  fedha hatimaye inazalisha ongezeko la fedha kwa wasimamizi wa miradi, hata wale wanaofanya hizo kazi wapo wanaochelewesha.

“Naiomba Wizara iunde kitengo maalumu kwa ajili ya kushughulikia miradi yote ya Rea kuepusha changamoto hizo,” amesema.

Aidha, mbunge huyo amehoji kuhusiana na mradi wa umeme wa Rufiji kwamba utatumia fedha nyingi wakati fedha hizo zingetumika kwenye miradi mingine kama ya jua.   

“Tumeambiwa itatumia miaka 10 ili lile bwawa liweze kujaa, Mheshimiwa Spika tunatumia hela nyingi kujenga mradi ambao utachukua muda mrefu na hautakuwa na faida.

“Maana yake tunataka kutengeneza historia kwani huo ni uharibifu wa fedha, tusipopata faida, tuna miradi ya jua na upepo, hizo trilioni 6.5 zilizotengwa, tungepeleka kwenye hiyo miradi mingine tungekuwa tuna umeme mwingi,” amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles