27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Mbunge ataka bungeni kifungwe kifaa cha kutambua wabunge wasiotahiriwa

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Viti Maalum Jacklin Ngonyani (CCM), ametaka bungeni kufungwe mashine maalum ya kukagua wabunge wa kiume ambao hawajatahiriwa.

Hayo aliyasema jana  bungeni wakati akichangia taarifa ya mwaka 2018-2019  ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi.

Mbunge huyo alisema ni vigumu kupambana na virusi vya ukimwi kama wanaume hawatofanyiwa tohara.

“Kuna virusi vinapatikana kwa wanaume wenye mkono wa sweta (wasiofanyiwa tohara). Natoa ushauri kufanyika vipimo kwa wabunge kubaini ambao hawakufanyiwa tohara,” alisema.

Kauli hiyo ilizua mjadala bungeni huku Spika wa Bunge, Job Ndugai, akieleza kuwa hoja hiyo haijaungwa mkono.

Uamuzi huo ulimfanya Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia, kuomba kutoa kutoa taarifa kwa spika ambapo alipopewa nafasi alimuomba Jackline kurudia tena hoja yake.

“Mheshimiwa Spika naomba kumpa taarifa mheshimiwa Mbunge arudie tena kutoa hoja yake ili tuiunge mkono kwa sababu wakati akizungumza tulikuwa hatusikii vizuri,” alisema.

Kabla ya Ngonyani kuendelea naye Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph  Musukuma  aliomba kutoa taarifa kwa spika.

Alipopewa nafasi, Musukuma aliibua hoja nyingine akitaka wakati ukaguzi kwa wanaume ukifanyika, pia ukaguzi kubaini wanawake waliokeketwa nao pia ufanyike.

“Mheshimiwa spika utafiti pia umebaini wanawake waliokeketwa nao wanachangia ongezeko la maambukizi ya ukimwi, sasa wakati wabunge wakiume wakipimwa pia upimaji ufanyike ukabaini waliokeketwa,” alisema ambapo wabunge waliangua vicheko akiwemo Spika.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,464FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles