27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Mbunge ashauri wananchi Tarime wasiibiane   mifugo 

Lameck AiroNa PETER FABIAN

MBUNGE wa   Rorya, Lameck Airo (CCM) amewataka viongozi na wananchi wa kabila la Wajaluo na Wakurya katika Kata za Koryo  wilayani  Rorya  na Bumera wilayani Tarime kutoibiana mifugo.

Amewataka  kuzika tofauti zao na kuendeleza ushirikianao, upendo na kuilinda amani iliyopo kwa maendeleo yao.

Kauli hiyo aliitoa  alipotembelea kata hizo jirani kwa lengo la kudumisha ujirani mwema baina ya viongozi na wananchi wake.

Alifanya ziara hiyo  baada ya   mapigano na mauaji ya wananchi makabila hayo yaliyotokea Juni mwaka 2009 wakituhumiana kuibiana mifugo na kusababisha amani kutoweka.

“Viongozi tusimamie na kudumisha amani na upendo lakini pia tuendeleze ushirikiano wetu kwa kuhakikisha tunailinda amani iliyopo.

“Hali hiyo itafanya  wananchi wa pande zote mbili waendelee na shughuli za maendeleo  ikizingatiwa kuna wakati   amani ilipotea na kukatokea machafuko ambako  watu walipoteza maisha,”alisema.

Alikuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Bumera (Tarime)  mpakani na Kata ya Koryo (Rorya) katika sherehe  zilizorejesha ngoma ya asili ya  wakurya baada ya kutochezwa kwa kipindi kirefu kutokana na mauaji yaliyofanya ngoma hizo kupigwa marufuku.

“Ombi langu kwa wote wa viongozi wa serikali za vitongoji, vijiji, kata na jimbo tukiwamo wawakilishi wa wananchi tusimamie amani  wananchi waendelee na shughuli za maendeleo.

“Tunatambua bila amani hakuna kitu maendeleo, hivyo rai yangu tuilinde amani tukatae wanaochoche na kutuvuruga kwa maslahi yao binafsi na tuwe wajasiri kutoa taarifa kwa viongozi wetu na vyombo vya dola ,”alisema.

Mbunge huyo   aliimarisha ujirani mwema kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji   baada ya viongozi wa kata hiyo kumweleza hali ya shule za msingi na sekondari kuwa ni  mbaya.

Walisema shule hizo zinahitaji kuboresha sakafu kwenye vyumba vya madarasa huku mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Tarime akichangia   Sh 500,000  na kumkabidhi Diwani wa Bumera, Marumi kwa ajili ya shule tano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles