30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mbunge amwangukia Waziri Lukuvi

ulegaNa Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

MBUNGE wa Mkuranga, Abdallah Ulega (CCM), amemwomba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Wiliam Lukuvi, kuhakikisha maeneo yaliyochukuliwa na wawekezaji bila kuendelezwa yanarudishwa kwa wananchi kwa mujibu wa sheria.

Hayo aliyasema jana, alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Magodani na Lugwadu mkoani Pwani, ambapo alisema maeneo yaliyohodhiwa na wawekezaji kwa muda mrefu bila kuendelezwa  sasa ni muda mwafaka kuyarejesha katika mikono ya wananchi.

Alisema pamoja na wawekezaji hao kupewa maeneo hayo lakini wameshindwa kuyaendeleza kwa muda wa miaka 20 na kusema hatua hiyo ni sawa na jipu linalosubiri kutumbuliwa.

Akizungumzia eneo la vijiji hivyo viwili lenye ekari 750 ambalo limekaa kwa muda mrefu bila kuendelezwa aliwataka wananchi  kuhakikisha wanasimama imara na kwenda katika Serikali ya kijiji ili waanze maandalizi ya kupata hati za maeneo yao.

“Fedha zitakazopatikana kuandikiwa hati ni vyema zikatumika kwenye masuala ya kijamii ikiwemo ujenzi wa shule kwani eneo hili halina shule iliyokaribu sote tu mashahidi, watoto wetu wanatembea kilomita sita hadi saba kufuata shule.

“Pia hakuna zahanati katika eneo hili wanakijiji mnaifuata Kongowe tunataka kuondoa unyonge huu,” alisema Ulega.

Alisema sheria ndogondogo za vijiji lazima zifuatwe katika kuhakikisha kwamba wanaendeleza maeneo hayo kwa maendeleo ya wilaya hiyo na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya kijamii ya TAMADA,  Abeli Mwakabenga,  alisema ni viongozi wachache ndio wenye moyo wa kusaidia kutetea maslahi ya wananchi lakini wengi wao wanatafuta masilahi yao binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,396FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles