30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AMTAKA WAZIRI AOMBE RADHI

Gabriel Mushi, Dodoma

Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe kuwaomba radhi Watanzania na Bunge kwa kudanganya kuwa fedha za maendeleo zilizotolewa katika bajeti ya mwaka 2017/18 ni asilimia 56 ilhali kamati ya bunge imebaini ni asilimia 22 tu.

Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo iliyowasilishwa leo bungeni jijini Dodoma, Kalanga amesema takwimu nyingi za taarifa za hotuba hiyo zinapingana na za Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Amesema waziri huyo ameonesha fedha za miradi ya maendeleo ya maji zimetolewa kwa asilimia 56 ili kulishawishi Bunge lipitishe bajeti hiyo ilihali wilaya nyingi ikiwamo Monduli hazijatengewa bajeti za mradi wowote mwaka huu.

“Waziri anasema ni asilimia 56 wakati kamati inasema 22, tunataka kujua nani ni mkweli? Amehoji Kalanga.

Akiwasilisha bajeti ya Mhandisi Kamwele katika bajeti ya mwaka 2017/18 hadi kufikia Machi mwaka huu wizara ilipokea fedha za maendeleo Sh bilioni 347.5 sawa na asilimia 56.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles