Mogadishu: Somalia
ALIYEKUWA mbunge Somalia, Salah Nuh Ismail (57) ametajwa kuwa mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga katika shambulio lililoua watu 13 mjini Mogadishu.
Mbunge huyo aliyekuwa anajulikana kwa jina la Badbaado, alijiunga na bunge la Somalia mwaka 2009 akiwa mmoja wa wabunge 275 waliochaguliwa na rais wa zamani, Sheikh Sharif Ahmed.
Alijiuzulu mwaka 2010 na kujiunga na al-Shabab baada ya kuwaita wabunge wenzake “makafiri”.
Katika tukio hilo kundi la ugaidi la Al Shabab limekiri kuhusika katika milipuko miwili ilitokea karibu na kambi ya vikosi vya Umoja wa Afrika (AU).
Al-Shabab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Afrika na jamii ya kimataifa.