31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge akabidhi vifaa vya kupimia corona

Allan Kitwe, Urambo

MBUNGE wa  Urambo mkoani Tabora, Magreth Sitta ametoa msaada wa vifaa vitatu vya kupimia joto ili kubaini watu wenye dalili za ugonjwa wa covid 19 katika hospitali ya wilaya hiyo vyenye thamani ya sh 1,350,000

 Sitta  alikabidhi vifaa hivyo (thermoscana tatu) juzi, ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona katika hospitali kuu ya wilaya hiyo. 

Alisema  awali alitoa vifaa vya kuoshea mikono pamoja na sabuni kwa wananchi walio katika mikusanyiko ya watu wengi, ikiwemo sokoni kama hatua ya kuunga mkono juhudi za halmashari ya wilaya hiyo katika kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

“Zipo hatua mbali mbali nilizochukua kama kiongozi ili kuunga mkono viongozi wenzangu wa halmashauri yetu, nilianza kutoa vifaa vya kunawia mikono na sabuni katika mikusanyiko, sasa nimeleta vifaa hivi ili kuwapima watu wote wanaoingia na kutoka hapa wilayani”, alisema.

Mganga Mkuu wa  wilaya hiyo, Dk. Paul Swakala alimshukuru Sitta kwa msaada huo na kuongeza  vifaa hivyo vitasawaidia mapambano ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Siasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Emanuel Kadelege alimpongeza Sitta  kwa kuziishi shida za wana urambo na kuwa karibu na wananchi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles