22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE AHOJI UHALALI WA BAKWATA KUWA MSEMAJI WA WAISLAMU

  • Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), amehoji uhalali wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuwa wasemaji wa waisalamu nchini.

    Akiomba mwongozo wa Spika bungeni leo Jumatatu Februari 5, Bobali alisema Waislamu wana madhehebu mengi lakini taasisi pekee ndiyo inayosikilizwa na serikali ni Bakwata.

    “Madhehebu mengine hayatambuliwi na hata ushiriki wa viongozi wakubwa wa kitaifa hawaonekani, Mheshimiwa Naibu Spika naomba mwongozo wako, hivi Bakwata ndiyo taasisi pekee iliyopewa mamlaka na serikali ya kuwaaemea waislamu wa nchi hii,” alihoji Bobali.

    Hata hivyo, akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alisema mwongozo huo umekosa sifa kwa mujibu wa kanuni ambapo zinamtaka muomba mwongozo kuzingatia jambo lililotokea bungeni na suala la Bakwata halijazungumzwa bungeni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles