22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge ahoji ongezeko la kodi za nywele bandia

Na Ramadhan Hassan-Dodoma

Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF) amesema kuna watu watawakimbia wake zao kutokana na kuongezeka kwa kodi katika nywele bandia.

Hatua hiyo, imekuja kufuatia bajeti ya 2019/20 kupendekeza ushuru wa bidhaa  kuwa asilimia 10 kwenye nywele bandia zinazotengenezwa ndani ya nchi na  asilimia 25 zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

Akichangia leo bungeni Juni 20,  bungeni katika Mjadala wa Bajeti Kuu, Khatibu amedai kwamba mungu alimuumba Adamu akaona dunia haipo vizuri hivyo akaamua kumleta Hawa ili mambo yakae vizuri.

“Mungu alimuumba Adamu akaona dunia zio nzuri akamleta Hawa leo mnamkamua? mimi nafanya kazi kumridhisha mwanamke,bila mwanamke nisingefanya kazi, mnatoza kodi ya wigi  kuna watu watawakimbia wake zao, ongezeni kodi kwenye pombe na sigara acheni mawigi wanawake wapendeze,”amesema huku Wabunge wakiangua vicheko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles