25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge aeleza sababu za kuangua kilio bungeni

MWANDISHI WETUDODOMA

MBUNGE wa Mlimba (Chadema), Suzan Kiwanga, ameeleza sababu za kuangua kilio bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Alisema  ni kutokana na adha ya  ubovu uliokithiri wa barabara ya Mlimba hadi mpakani mwa Mkoa wa Njombe eneo la Lwamote.

Akizungumza na MTANZANIA katika viwanja vya Bunge jana, Kiwanga alisema hali katika barabara hiyo ni mbaya mno na katika kipindi   cha mvua mabasi ya abiria yanayojaribu kwenda huko yanakaa njiani zaidi ya siku tatu huku abiria wengine wakiwa ni wagonjwa, watoto na wazee.

“Hivi ninavyoongea hata kijiko kilichokwenda kukwamua magari yaliyokwama na kusawazisha baadhi ya maeneo kwenye barabara hiyo kimezama, kuna basi lilikwama kwa siku tatu, wananchi wanataabika, nilipokumbuka  adha hizo na kujikuta ninatoa machozi.

“Kuna hatari watu wengine wanaweza kupata magonjwa ya mshutuko kama presha na hata kufia njiani  kwa sababu kama kijiko (katapila) kinazama unategemea nini kwa mabasi ya kwaida,”alisema Kiwanga.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa ubovu wa barabara hiyo  unaathiri masuala mtambuka yakiwamo  ya  uchumi na  jamii ikizingatiwa wananchi   wengi wanaoishi maeneo hayo ni wakulima na wazalishaji wakubwa wa mazao mbalimbali kama vile mpunga, ndizi, ufuta, kakao, mahindi pamoja na kilimo cha miti kwa ajili ya kulinda mazingira.

Alisema kwa sababu hiyo kukosekana  a barabara kunawasababishia zaidi umasikini.

Hata hivyo mbunge huyo alisema anashukuru waziri mwenye dhamana aliahidi kutatua kero hiyo ya muda mrefu na  tayari upembuzi yakinifu ulikwisha kufanyika tangu 2017 kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami kwa kuanzia Ifakara hadi Kihansi.

“Mbali na hiyo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 tunaishukuru serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi imetenga fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa kipande cha barabara ya Mlimba hadi Lwamote jambo ambalo ni hatua nzuri.

“Ni imani yangu na wananchi kwamba kero hiyo ya muda mrefu ya barabara hiyo inakwenda kupata ufumbuzi wa kudumu hivyo tusikate tamaa tuendelee kufanyakazi kwa bidii,”alisema Kiwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles