Mbunge aeleza sababu wananchi kusumbuliwa na Sumu kuvu

0
759
Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian

Mohamed Hamad

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian amesema wananchi wanakumbwa na tatizo la ugonjwa wa Sumu kuvu kutokana na wakulima kuvuna mahindi mapema kabla hayajakauka ili kuzuia yasiliwe na mifugo.

Anasema wakulima wanalazimika kuvuma mahindi yao mapema kutokana na kitendo cha baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao shambani kwa nguvu.

“Hili tatizo la Sumu tunaloona watoto wanapoteza maisha litaisha endapo hivi vitendo vya kulishiana mazao shambani vitakoma ili mkulima asubiri mazao yake yakauke ndipo avune kama ni huu utaratibu wa kuendelea kuviziana, kuchunga mashamba usiku lazima wavune tu yakiwa hayajakauka,” amesema Papian.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Taifa, Tevokatus Kasimba amesema watu nane kati ya 60 waliogundulika kuwa na sumu Kuvu mwaka huu wamepoteza maisha.

Amesema wamelazimika kwenda Kiteto ambako ni wakulima wazuri wa mazao aina ya mahindi na karanga ambayo ndio yanazalisha sumu hiyo kwa wingi kwa kuvunwa na kuhifadhiwa sehemu ambayo inazalisha sumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here